Huku bei ya mafuta ikiendelea kupanda kote duniani, Marekani inatafakari kuondoa baadhi ya vikwazo ilivyoweka kuhusu mafuta ya Iran.
Kulingana na Marekani, hatua hiyo inalenga kudhibiti bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa.
Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent, alisema hatu hiyo itawawezesha wanunuzi kwenye masoko ya kimataifa kupata mafuta.
Tangu Marekani na Israel zilipoanza kuishambulia Iran, bei ya mafuta katika soko la Kimataifa imekuwa ikipanda kila uchao.
Ikiwa hatua hiyo itatekelezwa, itakuwa ni afueni kubwa kwa mataifa mebgi duniani huku ikitarajiwa kufanikisha kupungua kwa bei ya mafuta.
Kabla ya vita hivyo kuanza, China ndiye alikuwa mnunuzi mkubwa wa mafuta ya Iran.