Marefarii watatu wa Kenya miongoni mwa 65 watakaosimamia kipute cha CHAN mwezi ujao

Dismas Otuke
1 Min Read

Marefarii watatu wa Kenya ni miongoni mwa waamuzi 65, ambao wameteuliwa na shirikisho la kandanda Afrika CAF,kusimamia kipute cha CHAN kati ya tarehe 1 na 28 mwezi ujao.

Kindumbwendumbwe cha CHAN kitaandaliwa kwa pamoja na Kenya,Uganda na Tanzania.

Dickens Mimisa Nyagrowa ndiye mwamuzi pekee wa kati kati ya uwanja aliyeteuliwa kati marefarii 26.

Samuel Mwangi Kuria atakuwa refa msaidizi huku Peter Waweru akiwa mwamuzi wa VAR.

Makala ya nane ya fainali za CHAN yataandaliwa Afrika mashariki kama matayarisho kwa fainali za AFCON mwaka 2027.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *