Waamuzi wa tatu wa Kenya ni miongoni mwa marefa watakaosimamia makala ya 34 ya fainali za kombi la mataifa ya Afrika AFCON nchini Ivory Coast kati ya Januari 13 na Februari 11 mwaka ujao.
Kwa jumela marefa walioteuliwa ni 68 wakiwemo waamuzi wakuu 26,wasaidizi 30 na maafisa wa VAR 12.
Waamuzi hao wanatarajiwa kuwasili mini Abdijan Ivory Coast kwa mafunzo kuanzia Januari 5 mwak 2024.
Peter Waweru Kamaku ndiye mwamuzi wa pekee wa kati kati ya uwanja aliyeteuliwa kutoka Kenya, huku Gilbert Cheruiyot na Stephen Yiembe wakiwa marefa wasaidizi.
Misri na Morocco ndizo nchi zilizo na marefa wakuu wengi wakiwa watatu kila moja, ilihali Mauritania na Gabon zinatoa marefarii wawili kila moja.