Marcel Sabitzer raia wa Austria amejiunga na Klabu ya Borrusia Dortmund Nchini Ujerumani kutokea klabu ya Bayern Munich.
Sabitzer 29, ambaye msimu Jana amekuwa Man United kwa mkopo anajiunga na Dortmund kwa mkataba wa Miaka minne.
Sabitzer alijiunga na Bayern Munich akitokea RB Leipzig mwezi wa Agosti mwaka juzi 2021 lakini akashindwa kuonyesha ubora wake Allianz Arena. Katika mechi 54, alifunga mabao mawili tu na kusaidia mawili akiwa na miamba hao wa Ujerumani.
Licha ya Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Austria kuonyesha nia ya kubaki Old Trafford, ilibainika wazi kuwa mchezaji huyo hakuwa Katika mipango ya Kocha mkuu wa Manchester United Erik Ten Hag, hivyo United iliondoa macho yake kwake na kuelekeza Kwa wachezaji wengine Kama vile Mason Mount ambaye alijiunga na mashetani hao wekundu Katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya joto.
🗣️💨 Medizincheck, Unterschrift und direkt auf zum ersten Interview. Festzuhalten bleibt: Marcel #Sabitzer hat Bock auf Dortmund, den BVB und die schwarzgelben Fans! 🤩
Die ersten Worte unseres Neuzugangs:
➡️ https://t.co/sWNGsXiVoA— Borussia Dortmund (@BVB) July 24, 2023
Akiwa na Vijana wa Erik Ten Hag Sabitzer alikuwa na msimu mzuri Kabla ya kupata jeraha la goti ambalo liliyumbisha na kumrudisha Nyuma lakini Sasa amepata makazi nyumbani kwa Mahasimu wa Bayern Munich, Signal iduna Park.
Sabitzer amejiunga na Dortmund kwa uhamisho wa pauni milioni 19.