Mabingwa mara saba wa kombe la Bara Afrika Misri ukipenda the Pharoes, walifuzu kwa raundi ya pili ya kombe la AFCON kimiujiza wakisajili sare ya tatu .
Mafarao walitoka sare ya mabao 2 dhidi ya Nyangumi wa Cape Verde na kuzoa pointi tatu, alama nne nyuma ya vionzi hao.
Hata hivyo nyota Ghana ambao wametwaa kombe hilo mara nne ilizimwa na Mambas wa kutoka Musumbiji,waliotoka nyuma magoli mawili na kulazimisha sare ya mabao 2 katika mechi ya kundi B.
Ghana waliyaaga mashindano kwa alama 2 mbili pekee.