Marais 16 wahudhuria Kongamano la Tabia Nchi Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guiterez

Takriban Marais 16 wanahudhuria kongamano la kwanza la Afrika kuhusu Tabia Nchi ambalo limeingia siku ya pili leo Jumanne katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi.

Kikao cha siku ya pili kinajadili jinsi ya kuongeza pesa zinazotengewa mijadala kuhusu tabia ya nchi katika mataifa ya Afrika na uwekezaji katika mazingira na utafiti anuai.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guiterez

Marais wanahodhuria kongamani hilo ni pamoja na Evariste Ndayishimiye kutoka Burundi, Nana Akufo Addo wa Ghana, Azali Assoumani wa Comoros, Brahim Ghali wa Sahrawi, Julius Maada Bio wa Sierra Leone, Sale Work Zewde kutoka Ethiopia, Isaias Afwerki wa Eritrea, Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini, Mohamed Younis wa Libya, Samia Suluhu kutoka Tanzania na Macky Sall wa Senegal.

Wengine ni pamoja na Filipe Nyus wa Msumbiji, Dennis Sassou Nguesso wa Congo, na Paul Kagame wa Rwanda.

Pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Antonio Guterres na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki.

Share This Article