Mapigano yazuka Ugiriki kati ya polisi na waandamanaji

Dismas Otuke
1 Min Read

Mapigano yalizuka nchini Ugiriki jana wakati waandamanaji walipokabiliana na polisi .

Hii ilifuatia hatua ya polisi kuingilia kati kuzima maandamano ya kuadhimisha miaka 16, tangu polisi walipomuua kijana mmoja na kusababisha maandamano mabaya zaidi nchini humo.

Yapata watu 5,000 walishiriki maandamano hayo yanayoandaliwa kila mwaka kukumbuka mauaji hayo ya kikatili ya kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 15.

Maelfu ya polisi walitumwa kushika doria huku zaidi ya raia 60 wakikamatwa .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *