Mapigano kati ya Israel na Hamas yaanza tena

Tom Mathinji
1 Min Read

Mapigano kati ya Hamas na Israel yameanza tena huko Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel limesema Ijumaa.

Kuanza tena kwa mapigano IDF imesema, kunafuatia Hamas kukiuka makubaliano ya muda na kundi hilo la wanamgambo kufanya shambulio la roketi dhidi ya Israeli.

IDF imesema kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, kwamba imefanikiwa kuzuia mashambulizi ya roketi kutoka Gaza.

Hakuna madai ya mara moja ya kuwajibika kutoka kwa Hamas kwa shambulio hilo la roketi.

Share This Article