Maonyesho ya kimataifa ya kilimo ya Nairobi (ASK) yataingia siku ya tatu leo Jumatano katika uwanja wa Jamhuri, huku idadi ya wanaotangaza bidhaa na kuzuru vibanda mbalimbali ikitarajiwa kuongezeka.
Maonyesho ya wiki moja yaliaanza juzi Jumatatu, Septemba 23 na yatakamilika Jumapili hii, Septemba 29.
Watu wazima wanalipishwa ada ya shilingi 300 na watoto shilingi 250.
Kampuni na mashirika mbalimbali yanatumia maonyesho hayo kutangaza bidhaa zao na kutoa hamasisho kwa wateja wanaotembelea vibanda vyao.