Manchester United wamekamilisha usajili wa mshambulizi wa Denamark Rasmus Hojlund kutoka Atalanta kwa pauni milioni 72.
Kinda huyo aliye na umri wa miaka 20 na aliyejiunga na Atalanta mwaka 2022 alifunga mabaoa 10 katika mechi 34 alizosakata msimu jana na amewasili ugani Old Traford kwa mkataba wa miaka mitano.
Mshambulizi huyo ni mwanandinga wa tatu kusajiliwa na meneja wa Man United Erik ten Hag msimu wa sasa wa uhamisho baada ya Mason Mount aliyetokea Chelsea kwa pauni milioni 55 na kipa Andre Onana kutoka Inter Milan kwa ada ya pauni milioni 47 nukta 2.