Man U yasuasua, Arsenal wavuna ushindi Ligi Kuu ya Uingereza

Martin Mwanje
1 Min Read
Mchezaji wa Man U Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Nottingham Forest / Picha kwa hisani ya BBC

Miamba wa soka nchini Uingreza Manchester United (Man U) waliendelea kusuasua kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo baada ya kulazwa na Nottingham Forest kwa bao 1-0 ugenini. 

Bao pekee la mechi hiyo iliyosakatwa jana Jumanne lilitiwa kimiani na Anthony Elanga, mchezaji wa zamani wa Man U.

Ushinde huo umewaacha Mashetani Wekundu, wanavyofahamika Man U, katika nafasi ya 13 kwenye jedwali la Ligi Kuu kwa alama 37 wakati Nottingham Forest ikishikilia nafasi ya 3 kwa alama 57, alama 4 pekee nyuma ya Arsenal.

“The Gunners” wanavyofahamika Arsenal walijiongezea alama tatu muhimu hiyo jana baada ya kuicharaza Fulham magoli 2-1.

Liverpool inaongoza jedwali la ligi hiyo kwa alama 70, ingawa wana mchezo mmoja zaidi wa kusakata na ikiwa wataushinda, watapanua pengo la alama kati yao na Arsenal hadi alama 12.

Liverpool wanapigiwa upatu wa kushinda Ligu Kuu ya Uingereza msimu huu kwani wameonyesha kumakinika sana mchezoni.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *