Masaibu ya klabu ya Manchester United yaliongezeka Jumamosi jioni baada ya kucharazwa mabao matatu kwa bila nyumbani na Bournemouth.
Mabao ya wageni yalipachikwa na Dominic Solanke,Philip Biling na Marcos Senesi .
Matokeo hayo yamewaacha Man U katika nafasi ya sita ligini huku wakijiandaa kwa mechi ya kufa kupona ya ligi ya mabingwa watakapowaalika Bayern Munich.