Makachero wamemkamata mwanamume mmoja anayeshukiwa kuongoza wizi wa simu za mkononi jijini Nairobi.
Wakati wa msako uliofanywa na maafisa hao, mamia ya simu za mkononi zilizoibwa zilipatikana.
Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI inasema mshukiwa kwa jina Jeremiah Mbugua, anaendesha duka la kuuza simu zilizotumika katika jumba la Califonia kwenye barabara ya Gaberone.
Mbugua alikamatwa kufuatia msako uliofanywa kwenye duka lake zilikopatikana simu hizo.
Kifaa cha kuweka programu na vifaa vya kuhifadhi data ni miongoni mwa vifaa vilivyopatikana wakati wa msako huo.
DCI inasema mshukiwa anazuiliwa na anawasaidia makachero katika uchunguzi.