Mamelodi wamlambisha shubiri Mwarabu Cairo na kuingia fainali

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ilifuzu kwa fainali ya kombe la Ligi ya Soka Afrika baada ya kulazimisha sare tasa dhidi ya Al Ahly ya Misri,katika mkumbo wa pili wa semi fainali uliosakatwa Alhamisi usiku mjini Cairo.

Mamelodi maarufu kama Masandawana waliokuwa wameshinda duri ya kwanza bao 1 kwa bila, watapambana na Wyad Casablanca ya Morocco, mkumbo wa kwanza wa fainali ukipigwa Novemba 5 mjini Casablanca, kabla ya kuwaalika Wydad tarehe 11 mwezi huu.

Mshindi wa kombe hilo atatuza shilingi milioni 600 huku timu ya pili ikiondoka na shilingi milioni 450.

Wydad walijikatia tiketi kwa fainali baada ya kuwashinda Esperance ya Tunisia, penati 5-4 kufuatia sare ya goli 1-1 baada ya mikondo miwili.

Share This Article