Mamelodi Sundowns watawazwa mabingwa wa AFL

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini ndio mabingwa wa makala ya kwanza ya kombe la African Football League, baada ya kuwashinda Casablanca ya Morocco mabao 3-2 kwa jumla.

Mamelodi almaarufu Masandawana walishinda duru ya pili ya fainali mabao 2 kwa bila mjini Pretoria Jumapili jioni.

Peter Shalulile aliwaweka wenyeji kifua mbele kwa bao la dakika ya ya tatu ya nyongeza ya kipindi cha kwanza, kabla ya Aubrey Modiba kutanua uongozi kwa goli la pili dakika ya 53.

Kufuatia ushindi huo Mamelodi wametia mkobani shilingi milioni 600 huku Wydad wakipokea milioni 450.

Share This Article