Mama Anne Nanyama Wetang’ula aliye mama yao Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula na Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi atazikwa leo .
Mwili wa mama Nanyama uliwasilishwa nyumbani katika kaunti ya Bungoma jana jioni tayari kwa mazishi ya leo.
Mama Nanyama,alizaliwa Machi 9 mwaka 1930 katika kijiji cha Sirare kaunti ya Bungoma na aliaga dunia Disemba 20 mwaka jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Viongozi wakuu serikalini wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo ya leo.