Mamake Mayorkun akanusha habari za mkasa wa moto

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa filamu za Nollywood Toyin Adewale ambaye pia ni mama mzazi wa mwanamuziki wa Nigeria Mayorkun, amekanusha taarifa kwamba kulikuwa na mkasa wa moto nyumbani kwa Mayorkun.

Taarifa hizo zilikuwa zimechapishwa na Galaxy Tv, na zilisema kwamba moto ulizuka nyumbani kwa mwimbaji huyo jijini Lagos Jumamosi usiku baada yake kurejea nyumbani.

Toyin anashangaa jinsi taarifa zinachapishwa tu bila kuzichunguza akisema yeye na familia yake wako salama na hawatarajii kukumbwa na tatizo lolote.

Anahisi kwamba taarifa hizo sio nzuri na ameombea dua familia yake.

Toyin hata hivyo alishukuru kila mmoja aliyewasiliana naye kwa ajili ya kumjulia hali akisisitiza kwamba wako salama kabisa.

Kulingana na chapisho la Galaxy TV kwenye Instagram, moto huo ulienea kwenye nyumba hiyo huku Mayorkun na familia yake wakiwa ndani na haijulikani iwapo waliondolewa humo salama.

Share This Article