Mama Taifa Rachel Ruto asema Rais hatakoma kutoa michango

Mama Rachel aliyekuwa akizungumza katika kanisa la AIC Pioneer jijini Eldoret, alisema alimfahamu Ruto kama mtu mkarimu hata kabla ya kuolewa naye, na amesalia hivyo kwa miaka 33 ambayo wamekuwa kwenye ndoa.

Marion Bosire
2 Min Read

Mama Taifa Rachel Ruto amesema kwamba Rais William Ruto hatakoma kutoa michango kanisani na kusaidia watu kwa sababu ni jambo alilozoea maishani.

Mama Rachel aliyekuwa akizungumza katika kanisa la AIC Pioneer jijini Eldoret, alisema alimfahamu Ruto kama mtu mkarimu hata kabla ya kuolewa naye.

Anasema kiongozi wa nchi amesalia mkarimu kwa muda wa miaka 33 ambayo wamekuwa kwenye ndoa. Kulingana naye, Rais anajali maslahi ya watu na hatabadilika sasa.

Mama taifa alihudhuria ibada ya shukrani ya kanisa hilo la AIC Pioneer jijini Eldoret ya kuadhimisha miaka 50 tangu kanisa hilo kuanzishwa.

Aliwataka waumini kutopoteza matumaini kwa sababu Rais Ruto anaongozwa na Mungu na kwamba hata ingawa mengi yanaende;ea nchini, wakenya wanastahili kuwa na imani kwamba nchi yao iko mahali salama.

Wito wake kwa viongozi wa dini na kanisa kwa jumla ni kuendelea kuombea taifa.

Alipongeza kanisa hilo la AIC Pioneer kwa kuwa kimbilio la matumaini,  chanzo cha chakula cha kirohona nguzo ya mabadiliko katika jamii kwa miongo mitano sasa.

Matamshi ya Mama Taifa yanajiri siku kadhaa baada ya viongozi wa kanisa katoliki kurejesha mchango uliotolewa na Rais William Ruto kwa kanisa moja huko Kayole.

Viongozi hao wa kanisa Katoliki nchini wanahisi kwamba michango kama hiyo kutoka kwa kiongozi wa nchi inalenga kuwanyamazisha wasizungumzie hali ilivyo nchini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *