Mama taifa Rachael Ruto awahimiza viongozi kaunti ya Narok kuungana

Tom Mathinji
1 Min Read
Mama Taifa Rachael Ruto.

Mama taifa Rachael Ruto ametoa wito kwa viongozi wa kaunti ya Narok kushirikiana na kuunga mkono vitengo mbali mbali vya uongozi, kwa manufaa ya kaunti hiyo na taifa nzima kwa jumla.

Aliwashauri viongozi kuweka pamoja hekima zao na kubuni suluhu za kudumu zitakazoleta maendeleo katika kaunti ya Narok.

Akizungumza wakati wa mkutano na viongozi katika uwanja wa Ole Ntimama katika kaunti ya Narok, Mama taifa aliwahimiza wanawake kuchukua fursa zinazojitokeza katika viwango vya kaunti na serikali ya kitaifa ili kuimarisha maisha yao.

Alisema serikali ya kitaifa imeyapa kipaumbele masuala ya wanawake akisisitiza hakuna yeyote wa kubaki nyuma.

Aidha Mama Taifa aliwahimiza wanawake kuanzisha kampuni watakazotumia kupata zabuni katika serikali za kaunti na ile ya kitaifa.

Alisisitiza ipo haja ya wanawake kutumia fursa kama hazina ya hasla ili kupata fedha za kupiga jeki biashara zao.

Mama Taifa alisema afisi yake inafanya kazi kuhakikisha maisha ya wnawake yameimarika kupitia vyama vya kina mama na kwamba serikali itahakikisha ujumuishwaji.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *