Timu ya taifa ya Kenya ya Voliboli kwa wanawake Malkia Strikers imeanza harakati za kuwania kombe la Afrika katika makala ya 21 kwa ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Rwanda Jumatano nchini Cameroon.
Malkia wameshinda kwa seti za 25-16,25-20 na 25-27 .
Kenya chini ya ukufunzi wa kocha Paul Bitok pia itamenyana na Morocco,Uganda, Burkina Faso na Lesotho katika kundi B .
Kundi A linasheheni Mali,Nigeria,Misri na Algeria,Burundi na wenyeji Cameroon.
Mashindano hayo yatakamilika tarehe 26 mwezi huu mjini Yaounde Cameroon.