Timu ya taifa ya mpira wa wavu ya wanawake almaarufu Malkia Strikers imewasili mjini Paris nchini Ufaransa siku ya Jumatatu, tayairi kwa mechi za ufunguzi katika makala ya 33 ya michezo ya olimpiki.
Malkia ni tiu ya pili kutua Paris baada ya ile ya raga kwa wanaume saba upande kutua Jumapili.
Timu hizo ziliwasili baada ya mazoezi ya takriban wiki moja mjini Miramas Ufaransa.
Shujaa iliwasili Paris katika kambi ya wanamichezo Jumapili tayari kwa mchuano wa ufunguzi kundini B dhidi ya Argentina Jumatano hii, na kisha kukabiliana na Australia baadaye usiku.
Kenya inayofunzwa na Kevin wambua itakamilisha ratiba ya mechi za kundi hilo Ijumaa hii dhidi ya Samoa.
Vidosho wa Voliboli watakita kambi ya mazoezi kwa wiki moja jijini Paris, kabla ya kuanza kibarua kundini B dhidi ya mibabe Brazil Jumatatu ijayo Julai 29.
Malkia watakumbana na Poland Julai 31 na kufunga ratiba ya mechi za makundi Agosti 3 dhidi ya Japan.