Malkia Strikers kuzindua uhasama dhidi ya Nigeria jijini Accra

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Voliboli kwa wanawake ya Kenya ukipenda Malkia Strikers ,itashuka uwanjani Jumamosi kwa mchuano wa kufa kupona dhidi ya Nigeria  katika michezo ya bara Afrika jijini Accra,Ghana.

Malkia walianza vyema kampeini ya kutetea taji baada ya kuichachafya Ushelisheli seti tatu kwa bila na ushindi dhidi ya Nigeria utaweka hai fursa ya kuongoza kundi hilo.

Kenya imejumuishwa kundi B na DR Congo,Algeria ,Ushelisheli na Nigeria huku kundi A likijumuisha Misri,Tunisia ,Gambia na wenyeji Ghana.

Website |  + posts
Share This Article