Mechi za raundi ya pili hatua ya makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya zilimalizika kwa kishindo huku timu limbukeni zikiwaangusha vigogo.
Aston Villa na Lille ya Ufaransa zilisajili ushindi wa bao 1 kwa bila kila moja dhidi ya Bayern Munich na mabingwa watetezi Real Madrid mtawalia.
Benfica ya Ureno ikiwa nyumbani pia iliwanyofoa Atletico Madrid kutoka Uhispania mabao 4 kwa bila.
Juventus ya Italia ilivuna ushindi wa magoli 3-2 ugenini kwa RB Leipzig ya Ujerumani,Liverpool ikaipepeta Bologna 2 bila jawabu ,Monaco na Dynamo Zagreb wakatoka sare ya 2-2 huku Club Brugge ikipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sturm Graz.