Makueni kuongoza mpango wa afya ya mifugo

Dismas Otuke
1 Min Read

Kaunti ya Makueni imechaguliwa na Serikali ya Kitaifa kuongoza mpango wa kitaifa wa Afya ya mifugo.

Mpango huo unanuia kuimarisha afya ya mifugo kupitia kampeini kamili za chanjo na kukuza ufugaji bora.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Makueni imefanikiwa kuchanja zaidi ya mifugo 400,000, wakiwemo ng’ombe, kondoo na mbuzi.

Juhudi hizo zililenga magonjwa kama vile ugonjwa wa Ngozi, Homa ya Rift Valley, Caprine Pleuropneumonia miongoni mwa mengine.

Mpango huo utatumika kama kielelezo kwa kaunti nyingine, ukionyesha mbinu mwafaka za kuboresha afya ya mifugo na tija kupitia chanjo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *