Makanisa kuanza kutozwa ushuru wa sadaka nchini Rwanda

Dismas Otuke
1 Min Read

Makanisa yataanza kutozwa ushuru wa sadaka na matoleo meningin nchini Rwanda, kama njia ya kuwazuia wahubiri bandia wanaowapunja waumini.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza haya baada ya makanisa takriban 8,000 kufungwa wiki iliyopita, kwa kutoafiki viwango vilivyowekwa na serikali.

Kulingana na Kagame kutozwa ushuru kwa sadaka,zaka na matoleo yote  ya kanisani kutoka kwa waumini kutaleta uzingativu wa sheria.

Halmashauri ya kuthibiti makanisa nchini Rwanda RGB, imesema kuwa asilimia 59.3 ya makanisa yaliyokaguliwa ambayo ni makaisa 13,000, hayajaafikia viwango vinavyohitajika.

Share This Article