Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Tundu Lissu ameachiliwa huru baada ya kukamatwa juzi na jeshi la polisi mkoani Arusha.
Jeshi hilo lilitangaza kumshikilia Lissu ambaye aliwahi kugombea urais katika uchaguzi wa 2020 kwa tuhuma za kufanya mikutano isiyokuwa halali na kuwazuia polisi kutekeleza majukumu yao.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linamshikilia Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mhe: Tundu Lissu pamoja na wenzake watatu wa Chama hicho kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za kufanya mikusanyiko isivyohalali na kuwazuia Askari Polisi kutekeleza majukumu yao,” ilisema taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo awali.
“Baada ya mahojiano hayo na ukamilishwaji wa taratibu zingine, hatua nyingine za kisheria zitafuata.”
Akizungumza na BBC, Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA John Mnyika amethibitisha kuachiliwa huru kwa Lissu.