Makamishna wapya wa IEBC kuapishwa Ijumaa

Tom Mathinji
1 Min Read
Jaji Mkuu na Rais wa mahakama ya upeo Martha Koome.

Mwenyekiti na Makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), wataapishwa leo Ijumaa katika Mahakama ya Upeo.

Uapisho huo unajiri baada ya makamishna hao kuteuliwa upya na Rais William Ruto kupitia gazeti rasmi la serikali, baada ya kesi iliyokuwa imewasilishwa mahakamani kupinga uteuzi wao kutupiliwa mbali.

Kwenye uamuzi uliotolewa Alhamisi alasiri, Majaji wa Mahakama Kuu waliharamisha ilani ya gazeti rasmi la serikali toleo la Juni 10,2025 iliyowateua makamishna hao, wakidai kuwa mahakama ilikuwa imetoa maagizo kwamba makamishna hao wasichapishwe kwenye gazeti rasmi la serikali.

Jaji Mkuu ataongoza hafla ya kuwaapisha Makamishna hao, huku wakikabiliwa na kibarua kigumu mbele yao zikiwemo chaguzi ndogo katika baadhi ya maeneo bunge na wadi ambapo viti vilisalia wazi kutokana na sababu toauti.

Watakaoapishwa ni pamoja na Mwenyekiti Erustus Ethekon Edung na Makamishna  Ann Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor Hassan, Francis Odhiambo Aduol na Fahima Araphat Abdallah.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article