Makala ya mwaka huu ya Ligi Ndogo kuandaliwa tarehe 17-18 Agosti

Tom Mathinji
1 Min Read

Makala ya mwaka huu ya kombe la Ligi Ndogo kanda ya Afrika mashariki, yameratibiwa kuandaliwa kati ya tarehe 17 na 18 mwezi Agosti mwaka huu Jijini Nairobi.

Mashindano hayo yatajumuisha vitengo mbali mbali, huku yakiwajumuisha wachezaji wa umri wa miaka saba hadi 19.

Mataifa kumi yamethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ya siku mbili yatakayoandaliwa katika  Nairobi Polo Club.

Wenyeji Kenya wanazialika timu kutoka Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, South Kusini, Somalia, Ethiopia, Sudan na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkurugenzi wa mashindano hayo Chris Amimo, ametoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwashabikia chipukizi wa mchezo wa soka, akielezea kuwa mashindano hayo yatavutia wachezaji wenye talanta za kupigiwa mfano.

“Sisi kama Ligi Ndogo, tumejitolea kutoa fursa kwa wachezaji kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa na hivyo kuwafungulia milango ya taaluma yao ya uchezaji wa soka,”alisema Amimo.

Miongoni mwa timu ambazo zimethibitisha kushiriki ni pamoja na UFA Simba (U7), Black Panthers (U9), Tanzania’s TeletubbiesKids League (U11), Legacy Football Academy (U13), na True Talents (U19).

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *