Makala ya 20 ya tuzo za SOYA kuandaliwa Machi mosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 20 tuzo za wanaspoti bora wa mwaka maarufu kama SOYA yataandaliwa tarehe moja mwezi ujao katika ukumbi wa KICC kaunti ya Nairobi.

Kulingana na mshiriki wa tuzo hizo John Kaplich Barsito hafla ya mwaka huu itaandaliwa hadi mwisho wa mwaka kwa shughuli mbali mbali kinyume na makala 19 ya wali.

Sherehe za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuongozwa na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya marathon Haile Gebreselasie kutoka Ethiopia zitakuwa na vitengo 16 tofauti vya washindi.

Tuzo za SOYA ziliasisiwa mwaka 2000 na Rais wa sasa wa kamati ya Olimpiki nchini Kenya NOCK Dkt Paul Tergat.

Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon na Eliud Kipchoge walitawazwa wanamichezo bora mwaka uliopita kwa wanawake na wanaume mtawalia.

Share This Article