Majeshi ya Israel yaangamiza Wapalestina 33 huku UN ikitaka mashambulizi kusitishwa

Dismas Otuke
1 Min Read
Familia zilizotoroka makwao nchini Syria

Wapalestina 33 waliuawa katika shambulizi la hivi punde lililotekelezwa na majeshi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikakati ya Ukanda wa Gaza huku 13 kati yao wakiuawa usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wanajeshi wa Israel wametekeleza mashambulizi ya angani eneo la Nuseirat na kuharibu makazi huku watoto wakionekana wakivuja damu baada ya kujeruhiwa na wengine wakifunikwa na vifusi vya majengo.

Yamkini watu 30 waliuawa na wengine takriban 50 kujeruhiwa.

Wakati uo huo, takriban watu milioni 1.1 wamehama makwao tangu kuzuka kwa mapigano kati ya majeshi ya Rais wa Syria Bashar al-Assad aliyeng’olewa mamlakani na makundi yaliyokuwa yakimpinga kuanzia tarehe 27 mwezi uliopita.

Majeshi ya Israel pia yameonekana yakiingia katikati kwa mji mkuu wa Syria, Damascus, yakiripotiwa kutekeleza mashambulizi tangu kubanduliwa mamlakani kwa Assad.

Umoja wa Mataifa, UN umeitaka Israel kusitisha mashambulizi hayo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *