Maafisa wa Polisi nchini Ufaransa wameanzisha uchunguzi wa wizi wa kimabavu uliotekelezwa na majambazi waliojihami nyumbani kwa kipa wa klabu ya Paris St Germain Gianluigi Donnarumma na mpenzi wake , Alessia Elefante, mapema Ijumaa.
Kulingnana na ripoti za awali majambazi hao walifika nyumbani kwa mchezaji huyo usiku wa manaene wakamfunga kwa kamba pamoja na mchumba wake kabla ya kutekeleza wiki huo.
Donnarumma na mchumbake walifanikiwa kutorokea katika mkahawa mmoja wa kifahari ulio karibu na baadae wakapelekwa hospitalini kutibiwa kwa mshtuko na majeraha madogo.
Wezi hao walitoroka na mikufu na saa za mkononi vya thamani ya shilingi milioni 78 za Kenya.
Wachezaji kadhaa wa PSG awali wameripotiwa pia kuibiwa wakiwemo Thiago Silva, Angel Di Maria, Eric Maxim Choupo-Moting, Presnel Kimpembe na Mauro Icardi.