Majaliwa amzuru Mkubwa Fella

Wakati wa ziara hiyo nyumbani kwa Fella, Majaliwa alimkabidhi msaada wa shilingi milioni 20.

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Kassim Majaliwa jana Julai 25, 2026 alimtembelea na kumjulia hali mdau wa muziki na mlezi wa vipaji nchini, Mkubwa Fella anayeugua.

Wakati wa ziara hiyo nyumbani kwa Fella, Majaliwa alimkabidhi msaada wa shilingi milioni 20.

Majaliwa alipata nafasi ya kufanya mazoezi mepesi ya viungo pamoja na Mkubwa Fella, ikiwa ni sehemu ya kumpa moyo katika kipindi hiki cha kuendelea kuimarisha afya yake.

Aidha, wawili hao walifanya mazungumzo kuhusu mchango wa Mkubwa Fella katika kukuza na kuendeleza muziki wa Tanzania, hususan katika kulea na kuinua vipaji vya Wasanii mbalimbali, pamoja na masuala mengine yanayohusu maendeleo ya tasnia ya sanaa Nchini.

Share This Article