Majaji sita walionyimwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta wamepewa malipo ya shilingi milioni 126 kama dhamana kwa ukiukaji wa haki zao za kimsingi.
Jaji Chacha Mwita amesema pesa hizo zinagharamia hasara ambayo sita hao walipata kisaikolojia baada ya Rais Mstaafu Kenyatta,kuwanyima fursa ya kufanya kazi licha ya kuidhinishwa na tume ya huduma za mahakama JSC.
Kenyatta kuwateua Majaji Aggrey Muchelule,Weldon Korir,Joel Ngungi na George Odunga kuwa majaji wa mahakama ya rufaa na Evans makori na Judy Omange kama majaji wa mahakama ya mazingira.
Rais mstaafu alikataa uteuzi wao kwa kisingizio cha kupata taarifa za ujasusi kuwa hawakustahili kupewa kazi hizo.
Jaji Mwita amemkosoa Rais mstaafu kwa kukiuka haki za majaji hao bila sababu maalum.