Majaji 20 wa Mahakama ya Juu waapishwa

Alphas Lagat
1 Min Read

Rais William Ruto  Leo Jumanne aliongoza hafla ya kuapishwa kwa majaji 20 wa Mahakama ya Juu katika Ikulu ya Nairobi.

Kuapishwa kwa majaji hao kulifanyika baada ya Rais Ruto kuchapisha majina yao kwenye gazeti rasmi la serikali mnamo Mei 9, 2024.

Tume ya Mahakama (JSC) ilikuwa imetuma majina ya majaji hao 20 kwa Rais baada ya kukamilika kwa mchakato wa mahojiano.

Majaji hao ni pamoja na Moses Ado Otieno, Alice Chepngetich Bett Soi, Benjamin Mwikya Musyoki, John Lolwatan Tamar, Francis Weche Andayi, Andrew Bahati Mwamuye, Julius Kipkosgei Ng’arng’ar, Wendy Kagendo Micheni na Emily Onyando Ominde.

Wengine ni Helene Rafaela Namisi, Alexander Muasya Muteti, Julius Mukut Nangea, Benjamin Kimani Njoroge, Caroline Jepyegen Kendagor, Stephen Nzisi Mbungi, Linus Poghon Kassan, Noel Onditi Adagi Inziani, Tabitha Ouya Wanyama, Rhoda Cherotich Rutto na Joe Omido Mkutu.

Msajili Mkuu wa Mahakama Winfrida Mokaya aliongoza hafla hiyo ya kuapishwa kwa majaji hao.

Waliokuwepo kwenye hafla hiyo ni Jaji Mkuu Martha Koome, naibu wake Philomena Mwilu, Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, Mkuu wa Sheria Justin Muturi, Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki miongoni mwa viongozi wengine.

Alphas Lagat
+ posts
Share This Article