Maina Njenga adai kutekwa nyara

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa kiongozi wa kundi haramu la Mungiki Maina Njenga anadai kutekwa nyara na watu wasiojulikana katika kaunti ya Kiambu Jumamosi usiku.

Kulingana na wakili wake Ndegwa Njiru Njenga alikamatwa na watesi wake akiwa nyumbani kwake.

Wakili huyo anadai kuwa kitendo hicho kilitekelezwa na maafisa wa idara ya uchunguzi wa kesi za jinai DCI.

Hata hivyo taarifa kinzani kutoka kwa ndunguye zadai kuwa Njenga alitekwa nyara na watu wasiojukikana kutoka kwa gari lake.

Share This Article