Aliyekuwa kiongozi wa kundi haramu la Mungiki Maina Njenga ameshtakiwa kwa kumiliki silaha butu na kuachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki moja.
Njenga amefikishwa katika mahakama ya Madaraka mapema leo Jumatatu.
Amedai kiini cha kukamatwa kwake na polisi ni hatua yake ya kujihusisha na siasa za eneo la Mlima Kenya.
Familia ya Njenga ilipaza sauti juzi Jumamosi ikisema Njenga alitoweka usiku baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana.
Taarifa za kuachiliwa kwake na watu hao zilichipuza jana Jumapili usiku kabla ya kufikishwa mahakamani leo Jumatatu.