Mahojiano ya kumtafuta mwenyekiti wa IEBC kukamilika Jumatano

Tom Mathinji
1 Min Read

Kamati ya kumtafuta mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchguzi na Mipaka (IEBC), itakamilisha mahojiano ya wawaniaji wa wadhifa huo leo Jumatano.

Miongoni mwa watu 11 walioorodheshwa kuwania wadhifa huo ni pamoja na wawaniaji watatu ambao ni, Joy Brenda Masinde-Mdivo, Ann Amadi na Lillian Wanjiku Manegene.

Hadi kufikia sasa wawaniaji wanane wamehojiwa, huku kundi la mwisho la wawaniaji watatu likihojiwa leo Jumatano. Watakaohojiwa Jumatano ni pamoja na Lillian Wanjiku Manegene (Kirinyaga), Robert Akumu Asembo (Busia) na Saul Simiyu Wasilwa (Bungoma).

Kamati hiyo ikiongozwa na Dkt. Nelson Makanda, imejukumiwa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa IEBC iliyoachwa wazi na marehemu Wafula Chebukati, aliyekamilisha muda wa kuhudumu. Chebukati alifariki mwezi Februari baada ya kuugua saratani ya akili.

Kamati hiyo imewahakikishia wakenya kwanza zoezi hil litatekelezwa kwa njia ya usawa na uwazi, na litahakikisha atakayeongoza tume hiyo atakuwa mwenye maadili ya hali ya juu.

Website |  + posts
Share This Article