Mahakama yasitisha miradi ya Adani katika kampuni ya KETRACO

Dismas Otuke
1 Min Read
Opiyo Wandayi - Waziri wa Nishati

Serikali imepata pigo baada ya mahaka kuu kusitisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya Kampuni ya Adani katika kampuni ya KETRACO

Jaji Bahati Mwamuye akitoa uamuzi Ijumaa amesema miradi yote chini ya makataba wa Adani na KETRACO, itasitishwa hadi pale uamuzi wa wa kesi iliyowasilishwa kupinga mkataba huo itakaposikizwa na kuamuliwa.

Jaji Wamunye pia ametoa agizo jingine la kuizuia wizara ya kawi kusaini mkataba mwingine na kampuni ya Adani  hadi uamuzi wa kesi iliyowasilishwa utakapotolewa.

Wizara ya kawi kupitia kwa shirika la KETRACO ilikuwa imesaini mkataba na kampuni ya India ya ADANI, wa kima cha shilingi bilioni 95 kwa kipindi cha miaka 30.

Share This Article