Wizara ya Afya imepewa siku 14 na mahakama ili kutafuta suluhu mwafaka kwa mgomo wa madaktari unaondelea kote nchini.
Jaji wa mahakama kuu Byrum Ongaya ametoa uamuzi huo Jumatano baada ya kuskiza pande zote mbili,walalamishi wakiwa Wizara ya Afya na mshtakiwa wakiwa ni Madaktari wanaowakilsihwa na chama cha KMPDU.
Kulingana na agizo hilo Madaktari watasitisha tu mgomo, baada ya pande zote mbili kuwasilisha mwafaka wa makubaliano .
Hospitali Kuu ya Kenyatta ambayo pia iliwakuwa imewashitaki madaktari, imesema kuwa haina uwezo wa kusubiri kwa majuma mawili kwani wagongwa wanaendelea kufariki.
Mgomo huo umeingia wiki ya tatu huku huduma za matibabu zililemazwa katika hospitali zote za umma.