Mahakama ya upeo yatupa nje kesi ya jaji Chitembwe

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya upeo imetupilia mbali kesi ya rufaa iliyowasilishwa na jaji wa mahakama kuu Said Juma Chitembwe, iliyopinga kutimuliwa kwake na jopo la majaji lililobuniwa kumchunguza.

Mahakama hiyo imedumisha uamuzi wa awali uliompa jaji huyo na makosa ya kukiuka kanunui za utendakazi kwa majaji.

Benchi ya majaji watano inayowajumuisha Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaac Lenaola na William Ouko imempata chitembwe kukiuka maadili ya utendakazi.

Uamuzi huo una maana kuwa Jaji Chitembwe hana fursa ya kurejea tena afisini.

Share This Article