Mahakama kuu yasimamisha utoaji wa vitambulisho vya kidijitali

Marion Bosire
1 Min Read

Mahakama kuu imesimamisaha utoaji wa vitambulisho vipya vinavyojulikana kama “Maisha Card”, hadi pale ambapo kesi ya kuvipinga itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Jaji John Chigiti ameelekeza serikali kukomesha usajili wa wakenya kwa ajili ya vitambulisho hivyo kufuatia kesi iliyowasilishwa na Katiba Institute.

Chigiti katika uamuzi wake alisema kwamba baada ya kupitia stakabadhi zote zilizowasilishwa na mlalamishi, amethibitisha kwamba ni kesi ambayo inastahili kusikilizwa na kuamuliwa.

Alitaja kesi hiyo kuwa inayopaswa kusikilizwa haraka huku akielekeza mlalamishi ambaye ni Katiba Institute kuwasilisha stakabadhi za kesi kwa mshtakiwa ambaye ni waziri wa mambo ya ndani na ushirikishi wa shughuli za serikali kuu katika muda wa siku saba.

Washtakiwa kwenye kesi hiyo na watu wengine ambao wangependa kujumuishwa wana muda wa siku 14 kuwasilisha majibu yao mahakamani.

Kesi hiyo itatajwa Februari 6, 2014.

Share This Article