Mahakama Kuu yakataa kusimamisha mchakato wa kumtimua Gachagua

Tom Mathinji
1 Min Read
Mahakama Kuu hapa nchini imekataa kwa mara ya pili kutoa maagizo ya kusimamisha mchakato unaotekelezwa na bunge la taifa, wa kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Swala hilo lilitajwa leo Jumatatu mbele ya Justice Bahati Mwamuye, aliyeagiza kesi hiyo iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha UDA Cleopas Malalah, lipelekwe mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Chacha Mwita kwa mwelekeo zaidi.

Mnamo Septemba 30, 2024, mahakama ilikataa kutoa maagizo ya kuzuia bunge kujadili hoja ya kumuondoa mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Kesi hiyo iliyosimamishwa na Malala, ilitaka bunge la taifa na lile la Senate, kuzuiliwa kuwasilisha, kujadili au kutekeleza hoja yoyote inayolenga kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Malala alidai kuwa mabunge hayo mawili hayajatimiza hitaji la uwakilishi wa thuluthi mbili wa kijinsia, na hivyo yamebuniwa kinyume cha katiba.

Share This Article