Mahakama kuu nchini Romania imefutilia mbali matokeo ya kura za Urais kufuatia madai ya Urusi kuingilia kati uchaguzi huo kumaanisha kuwa shughuli hiyo itarejelewa tena .
Raundi ya pili ya uchaguzi huo ilipangiwa kuandaliwa Jumapili hii kufuatia matokeo hayo yaliyoashiria hakuna mgombeaji aliyeshinda katika raundi ya kwanza.
Serikali sasa itatangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo .
Duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliopangiwa Jumapili hii ulikuwa kati ya waaniaji wawili Calin Georgescu,wa mrengo wa kulia , dhidi ya Elena Lasconi anayeungwa mkono na mataifa ya Ulaya.
Uamuzi huo mahakama kuu umeiacha nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kikatiba, huku muda wa kuhudumu kwa Rais wa sasa ukikamilika Disemba 21.