Mahakama Kuu imetangaza kwenda mapumzikoni kati ya Agosti 1 na Septemba 15 mwaka huu.
Mapumziko hiao pia yatashirikisha mahakama za uajiri na utatuzi wa mizozo ya wanyakazi na mahakama ya mazingira na ardhi.
Kulingana na katiba ya Kenya kifungu cha 165(1) sehemu ya 10(1) 2(a), Mahakama Kuu iko huru kwenda mapumzikoni kwa kuchapisha arifa kwenye gazeti la serikali.
Jaji Mwandamizi Eric Ogola amesema watatumia mapumziko hayo kuwateua majaji watakaosikiza na kutoa uamuzi wa kesi.
Hata hivyo, ofisi za mahakama hizo zitafunguliwa kwa umma kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni siku za kufanya kazi.