Majaji watatu wa mahakama huu siku ya Alhamisi wanatarajiwa kutoa mwelekeo wa kesi inayopinga kuanzishwa kwa mtaala wa elimu ya umilisi, CBC.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na wakili Nelson Havi inatarajiwa kutolewa kufuatia hatua ya Rais William Ruto, kuunda tume ya kuchunguza dosari zilizopo mwezi Septemba mwaka uliopita.
Mahakama pia itajulishwa endapo afisi ya mwanasheria mkuu iliwasilisha ripoti ya mapendekezo ya jopo la Rais.
Havi alikuwa amemshtaki aliyekuwa Waziri wa Elimu marehemu Prof. George Magoha, hali iliyolazimisha mahakama kuwashurutisha washtaki kuondoa jina na marehemu waziri kabla ya kuendelea.