Mahakama ya Juu kutoa mwelekeo kuhusu sheria ya fedha Agosti 28

Tom Mathinji
1 Min Read

Mahakama ya Juu tarehe 28 mwezi huu itatoa mwelekeo kwenye kesi iliyowasilishwa na Seneta wa kaunti ya Busia Okiya Omtatah ya kupinga agizo la mahakama la kuruhusu utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023.

Naibu msajili wa hiyo Bernard Kasavuli amesema kesi hiyo itatajwa kupitia kwa mtandao siku hiyo ambapo mwelekeo utatolewa.

Kasavuli amemuagiza Omtatah kumkabidhi Waziri wa Fedha  Njuguna Ndung’u na wengine kumi taarifa za rufaa iliyowasilishwa katika mahakama hiyo.

Kwenye rufaa hiyo, Omtatah anasema itakuwa vigumu kurekebisha madhara yaliyosababishwa na utekelezaji wa sheria hiyo mpya baada ya kuidhihirishia mahakama jinsi Wakenya walivyoathiriwa na kile alichotaja kuwa mfumo wa utozaji ushuru unaokiuka katiba.

Anaitaka Mahakama ya Juu isimamishe maagizo ya Mahakama ya Rufaa yaliyoruhusu utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *