Mahakama kutoa uamuzi juu ya ubomozi wa nyumba Mavoko

Martin Mwanje
1 Min Read

Mahakama ya Mazingira na Ardhi leo Alhamisi itatoa uamuzu kuhusiana na ombi lililowasilishwa na wanachama wa kundi la Aimi Ma Lukenya la kutaka ubomozi wa nyumba unaoendelea katika eneo la Mavoko kusitishwa. 

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa majira ya saa kumi jioni.

Na huku zikiwa zimesalia saa chache kabla ya uamuzi huo kutolewa, mahakama pia inatarajiwa kutoa maelekezo kuhusu ombi la serikali ya kaunti ya Machakos kutaka kujumuishwa kwenye kesi hiyo.

Ubomozi huo wa nyumba ulianza baada ya mahakama kubaini kuwa ardhi zilikojengwa nyumba hizo ni ya kampuni ya saruji ya East African Cement Portland, EAPC.

Serikali ya kaunti ya Machakos chini ya uongozi wa Gavana Wavinya Ndeti imelaani vikali ubomozi huo ikiutaja kuwa wa kinyama.

Aidha upande wa upinzani sawia na baadhi ya viongozi wa kidini wamelaani ubomozi huo wakilalamikia mahangaiko ya raia wasiokuwa na hatia ambao sasa wameachwa bila makazi.

Wakenya wengi wanakadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya nyumba zao zilizosemekana kujengwa kwenye ardhi hiyo ya EAPC kinyume cha sheria kubomolewa.

Share This Article