Mahakama: Jowie ndiye aliyemuua Monicah Kimani

Martin Mwanje
1 Min Read

Mahakama imebaini kuwa Joseph Irungu almaarufu Jowie ndiye aliyemuua mfanyabiashara Monicah Kimani. 

Marehemu Kimani alipatikana ameuawa katika makao yake ya Lamuria Gardens, karibu na barabara ya Dennis Pritt mwaka 2018 mtaani Kilimani.

Katika hukumu yake, Jaji Grace Nzioka amesema upande wa mshtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kudhihirisha kuwa ni Jowie aliyetekeleza mauaji hayo.

Alitoa mfano wa Jowie kuiba kitambulisho cha kitaifa cha Dominic Bisera, kuvaa kanzu na kisha kuficha utambulisho wake alipoelekea katika makao ya marehemu huko Lamuria Gardens alikotekeleza mauaji hayo na kisha kuondoka.

Mahakama sasa inatarajiwa kutoa kifungo atakachokitumikia Jowie Machi 8, 2024.

Hata hivyo, mwanahabari Jackie Maribe ameondolewa mashtaka ya mauaji yaliyomkabili.

Hii ni baada ya Jaji Nzioka kusema upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kudhihirisha Maribe alihusika katika mauaji hayo.

Hata hivyo, Jaji Nzioka aliitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kumfungulia mashtaka Maribe kwa kutoa ushuhuda wa uongo.

 

 

 

Website |  + posts
Share This Article