Magavana wanaitaka wizara ya afya ilipe deni la shilingi bilioni 8 ambazo hospitali za kaunti zinaidai kupitia kwa bima ya NHIF, kabla ya kaunzisha bima mpya ya SHA Julai mosi.
Mwenyekiti wa Magavana Ann Waiguru alifanya kikao na Waziri wa afya Susan Nakhumicha kutafuta suluhu kuhusu tandabelua hiyo wiki moja kabla ya kufungwa kwa matumizi ya NHIF.
Mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraaza la Magavana Muthumi Njuki, amesisitiza kuwa iwapo wizara ya afya haitalipa madeni hayo kabla ya Julai mosi ,hospitali nyingi za kaunti zitashindwa kutoa huduma.
Wakati uo huo Magavana wameteta hatua ya hazina kuu kupunguza mgao wa pesa kwa kaunti kwa shilingi bilioni tano ilivyopendekeza katika bajeti ya mwaka 2024,2025.
Waiguru amesema kukata bajeti hiyo kutadumaza huduma na miradi ya maendeleo katika kaunti.