Magavana washutumu kukamatwa kwa Gavana Godhana

Dismas Otuke
1 Min Read

Baraza la Magavana nchini (CoG) limeshutumu vikali kukamatwa kwa Gavana wa Tana River Dhadho Godhana. 

Godhana alikamatwa jana usiku kutoka nyumbani kwake na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI.

Kwenye taarifa, mwenyekiti wa CoG Ahmed Abdullahi amesema haki za Gavana Godhana zilikiukwa kwa jinsi alivyokamatwa.

Baraza hilo limesisitiza kuwa DCI walipaswa kumuita Gavana Godhana badala ya kumkamata kwa njia ya kumkosea heshima.

Limeongeza kuwa litashirikiana na Wizara ya Usalama wa Kitaifa kuhakikisha Gavana Godhana anatendewa haki.

TAGGED:
Share This Article